England ukingoni kushindwa katika mtihani wa kwanza wa kriketi

Chanzo cha picha, Getty Images
England ipo ukingoni kushindwa katika mtihani wa kwanza baada ya Australia kuendelea kung'ara kwa siku ya nne Brisbane.
Ikiwa inahitaji pointi 170 ili ishinde, timu hiyo mwenyeji inahitaji pointi 56 pekee Jumatatu, kufika mwisho wa pointi 114-0, David Warner akiwana pointi 60 na Cameron Bancroft akiendelea pasi kushindwa kwa pointi 51.
Shabaha ya pointi hizo imetokana na kazi nzuri ya warushaji mpira walioiondoa England kwa 195.
England ilikuwa na nafasi ya kuipa changamoto zaidi Australia lakini Joe Root (51), Jonny Bairstow (42) na Moeen Ali (40) walishindwa kutoa mchango mzuri baada ya mwanzo mzuri.
Baada ya Moeen kushindwa kudhibiti mipira ya Nathan Lyon, Ilibidi England ifyate mkia kutokana na umahiri wao Mitchell Starc na Pat Cummins.
Na matuamaini yoyote ya England kuikasirisha Australia yaliondolewa na Warner na Bancroft, walionyaka mipira na kutoa adhabu ya kisawa sawa ilioongeza matumaini ya kumaliza kwa ushindi kwa siku ya nne mtawalaia.
Muda ulikwisha lakini Jumatatu Australia itakwea kwa pointi 1-0 katika azimio lao la kushinda taji na kuhifadhi rekodi ya kutoshindwa katika Gabba tangu mnamo 1988.








