Habari za Global Newsbeat 1500 16/04/2018
Iliyochapishwa
Nyota wa Wrestling John Cena na mpenzi wake Nikki Bella wametangaza kuwachana. Nikki aliandika kwenye ukurasa wake wa Twitter kwamba uamuzi huo ulikuwa mgumu lakini bado wanapeana heshima. Walitarajiwa kufunga ndoa tarehe tano mwezi ujao. Je, kuolewa na mtu mliye kwenye taaluma moja ni vigumu zaidi?
Tupe maoni yako kwenye ukurasa wetu wa Facebook BBCNews Swahili