Tetesi za Soka Ulaya Jumanne 21.04.2020: Kane, Sancho, Mbappe, Partey, Aubameyang

Chanzo cha picha, Getty Images
Kiungo wa kati wa zamani wa timu ya Liverpool Graeme Souness amewaonya Manchester United wana hatari ya ''kudhalilishwa'' kama wamefanya makubaliano na winga Jadon Sancho (20) bila ya klabu yake ya Dortumund kuhusika. (Daily Mirror)
Manchester United hawataweza kumnunua mchezaji ghali kama mshambuliaji wa Spurs Harry Kane,26, wakati wakifikiria tena mikakati yao ya uhamisho kwa sababu ya hali ya fedha kutokana na mlipuko wa virusi vya corona. (Guardian)
Hata hivyo wacheza kamari wanaipigia chapuo zaidi United kumsaini Kane pamoja na Sancho,20. (Evening Standard)

Mshambuliaji wa Paris St-Germain Kylian Mbappe, ambaye amehusishwa na uhamisho wa pauni milioni 250 kwenda Real Madrid, huenda gharama ya uhamisho wake ikashuka mpaka pauni milioni 35 kwa sababu ya janga la corona, kwa mujibu wa mbunge wa zamani wa Bunge la Ulaya. (Daily Mirror)
Kiungo wa kati wa Atletico Madrid na raia wa Ghana Thomas Partey anatazamwa kwa karibu na kocha wa Arsenal Mikel Arteta, lakini klabu hiyo ya Uhispania inaamini kuwa inaweza kuendelea kumshikilia mchezaji huyo, 26 kwa mkataba mpya. (Express)

Chanzo cha picha, Getty Images
Manchester City wamedokezwa kujiunga kwenye kinyang'anyiro cha kumnasa mshambuliaji wa Arsenal Pierre-Emerick Aubameyang huku Barcelona, Inter Milan na Real Madrid nao wakitaka kumnyakua mchezaji huyo ambaye atamaliza mkataba wake mwaka 2021. (Express)
Manchester United wameachana na mipango yao ya kumfuatilia kiungo wa Real Madrid na Colombia James Rodriguez, lakini Arsenal na Everton wanavutiwa. (Sky Sports, via the Sun)

Chanzo cha picha, Getty Images
Mchezaji anayelengwa na Manchester City Kalidou Koulibaly, 28 , ambaye pia anahusishwa na taarifa za kunyemelewa na Paris St-Germain, amesema angependa zaidi kuhamia England, lakini kukaa kwake Italia ni suala la uamuzi wa mchezaji beki huyo wa kati wa Napoli. (Le10Sport, via Sports Illustrated)
Kiungo wa Manchester City David Silva, 34, yuko kwenye mazungumzo na klabu ya zamani ya Valencia na mkataba wake unatarajiwa kukamilika tarehe 30 mwezi Juni, lakini makubaliano hayo yamekuwa magumu kutokana na mlipuko wa virusi vya corona. (ESPN, via Manchester Evening News)
Silva amewataja wachezaji wanne wa Manchester United waliotoa upinzani mkali alipokabiliana nao Ryan Giggs, Paul Scholes na ndugu wa Neville , Gary na Phil. (Daily Mirror)












