Tetesi za soka Ulaya Jumatatu tarehe 29.06.2020: Koulibaly, Pochettino, Skriniar, Hakimi, Moreno, Tagliafico

Chanzo cha picha, Getty Images
Liverpool wameripotiwa kuwa wako mbele ya Manchester City katika kinyang'anyiro cha kumsaka kiungo wa kati-nyuma Msenegal Kalidou Koulibaly, 29, ambaye kwa sasa anachezea klabu ya Napoli kwa kumtoa Mcroasia Dejan Lovren, anayecheza safu ya ulinzi akiwa na umri wa miaka 30, kama sehemu ya uhamisho. (Tuttosport via Sun)
Mkurugenzi mkuu wa wakurugenzi Giuseppe Marotta anasema kuwa " mazungumzo ya klabu yamefikia kiwango cha juu" kwa ajili ya mchezaji wa Borussia Dortmund anayecheza kwa mkopo Achraf Hakimi huku beki wa huyo wa Real Madrid Mmorocco , 21, na kikaribia kuwa na uwezekano wa kuhamia serie A. (Goal)

Chanzo cha picha, Getty Images
Chelsea imepata msukumo wa uhamisho kwa meneja wa Ajax - Erik ten Hag kupendekeza kuwa difenda wa Argentina Nicolas Tagliafico mwenye umri wa miaka 27 na mlindalango wa Cameroon Andre Onana, mwenye umri wa miaka 24, wanaweza kuondoka kwenye klabu hiyo msimu huu huku kiungo wa kati wa Uholanzi Donny Van de Beek, anayelengwa na Manchester United akisemekana lkuwa huenda pia akaondoka katika klabu hiyo. (Express)

Manchester City wamejipanga kusaini mkataba na mshambuliaji wa Juventus Muhispania Pablo Moreno, mwenye umri wa miaka 18, katika dili ya kubadilishana mchezaji huyo ambayo itamuwezesha winga Felix Correia, mwenye umri wa miaka 19, kuhamia upande mwingine. (Goal)

Chanzo cha picha, Getty Images
Inter Milan wanaangalia uwezekano wa kumuuza Mslovakia difenda Milan Skriniar, 25, msimu huu huku Manchester City wakiwa ni miongonbi mwa wale wanaomtaka. Mchezaji wa safu ya mashambulizi wa City Muargentina Sergio Aguero, 32, anaweza kuwa sehemu ya kuweno katika mkataba huo . (Calciomercato - in Italian)
Benfica wanaripotiwa kuwa wanataka kumteua meneja wa zamani wa Tottenham Hotspur Mauricio Pochettino kama meneja wao mpya . Akiwa na umri wa miaka 48 Pochettino amekua nje ya uwanja tangu Novemba mwaka jana. (Record - in Portuguese)

Mshambuliaji wa zamani wa Ivory Coast na Chelsea Salomon Kalou, 34, ambaye mkataba wake unaisha katika Hertha Berlin mwishoni mwa msimu , anakaribia kukubali uhamisho wa bure katika timu ya Brazil ya Botafogo. (Yahoo Sports)
Torino wako tayari kumuuza difenda Mnigeria Ola Aina kwa Everton andna West Ham miongoni mwa timu zinazomtaka kijana huyo mwenye umri wa miaka 23. (Inside Futbol)

Winga Mmarekani Konrad de la Fuente mwenye umri wa miaka 18 amesaini makubalian ya kurefusha mkataba wake katika Barcelona tambao una kipengele cha kumuachilia cha thamani ya euro milioni 100 (£91m) iwapo atapata timu nyingine ya kuhamia ya daraja la kwanza. (AS

Chanzo cha picha, Getty Images
Mabigwa wapya wa ligi ya Premia, Liverpool wanajiandaa kumnunua beki wa Napoli Kalidou Koulibaly, 29, katika siku chache zijazo. (Tuttomercato, via Mail)
Kocha wa Bayer Leverkusen, Peter Bosz amethibitisha kuwa mkataba wa Kai Havertz kuondoka klabu hiyo huenda ukakamilishwa kufikia mwezi Augosti, huku wChelsea, Real Madrid na Manchester United wakiwa miongoni mwa klabuzinazomng'ang'ania mshambuliaji huyo wa Ujerumani mwenye umri wa miaka 21. (Sun)












