Tetesi za Soka Ulaya Jumanne 11.08.2020: Sancho, Ramsey, Smalling, Havertz, Traore, Hendrick

Aaron Ramsey

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kingo huyo wa kati wa kimataifa wa Wales Aaron Ramsey (kushoto)akishangilia bao Arsenal
Iliyochapishwa

Aaron Ramsey hajamridhisha kocha Andrea Pirlo wa Juventus. Kingo huyo wa kati wa kimataifa wa Wales mwenye umri wa miaka 29 yuko huru kuhamia klabu nyingine. (Mirror)

Inter Milan wanamlenga beki wa Manchester United Chris Smalling, 30, wakati wa uhamisho. (Gazzetta dello Sport)

Manchester United wanaendelea na juhudi za kumsaka winga wa kimataifa wa England Jadon Sancho licha ya Borussia Dortmund kusisitiza kuwa nyota huyo wa miaka 20- atasalia katika klabu hiyo msimu ujao. (Mail)

Jadon Sancho

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Winga wa kimataifa wa England Jadon Sancho

Kiungo wa kati wa JuventusBlaise Matuidi, 33, atajiunga na Inter Miami inayoshiriki ligi ya MLS akisubiri akisubiri matokeo ya uchunguzi wa kimatibabu . (Goal)

Arsenal wanakaribia kukamilisha mchakato wa kumsajili kiungo wa zamani wa Chelsea Willian,32, baada ya nyota huyo wa Brazil kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu. (Standard)

Chelsea wamekubali kumpatia mkataba wa miaka mitano mshambuliaji wa Bayer Leverkusen na Ujerumani Kai Havertz lakini wamefahamishwa kuwa kiungo huyo wa miaka 21- atawagharimu £90m. (RMC Sport - via Sun)

Kai Havertz

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Chelsea wako tayari kumnunua mshambuliaji wa Bayer Leverkusen na Ujerumani Kai Havertz

Chelsea wanakakabiliwa na ushindani mkali kutoka kwa Lazio katika kinyang'anyoro cha kumsaini beki wa Real Madrid Mhispania Sergio Reguilon, 23. (DiMarzio)

Manchester City watapokea ada ya £8m kumuachilia mlinzi wa kati wa Argentina Nicolas Otamendi,32, msimu huu wa joto. (Sun)

Newcastle wanajiandaa kumenyana na AC Milan na Roma kumsajili kiungo wakati wa Burnley Jeff Hendrick, 28. (Guardian - via Mail)

Nicolas Otamendi

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Manchester City kumuuza beki wao Nicolas Otamendi

Wolves wana imani mkufunzi wao Nuno Espirito Santo atasaini mkataba mpya kabla ya msimu mpya wa ligi kuu ya primia. (90Min)

Leicester City wanamfuatilia winga wa Barcelona na Portugal Francisco Trincao, 20. (Fabrizio Romano - via Leicester Mercury)

Aston Villa na Crystal Palace wamehusishwa na uhamisho wa kiungo mahiri wa Norwich Muargentina Emiliano Buendía, 23. (HITC via Sun)