Andropause: Kwanini hisia za kujamiiana hupungua kwa baadhi ya wanaume? Ni chakula gani chenye vitamini zinazoongeza uzalishaji wa homoni?

ప్రతీకాత్మక చిత్రం

Chanzo cha picha, Getty Images

Iliyochapishwa

Mara ya kwanza ilidhaniwa kuwa yalikuwa ni mabadiliko yaliyotokana na umri. Lakini kukosa subira kwake hakuishi kabisa na kikume chake hali hii inaongezeka siku hadi siku.

"Hata watu wengine wanamkwepa wanasema kuwa hawataki kuwa karibu naye wala kumgusa. Je unanipenda au hapana? Sijui kama ninapenda ngono au hapana ,"alisema Shailaja.

"Ingawa kwa kawaida ananiamini , kwa sasa amekuwa kama mtu mpya kwangu chumbani.

Akiwa na umri wa miaka 50, Shailaja anakabiliwa na tatizo la kushuku kuwa mume wake anaweza kuwa na uhusiano wa kimapenzi nje ya ndoa .

Ni kitu cha kwenda kwa daktari kujadiliana? Tatizo la kiakilini kwamba ameshindwa kupata suluhu. Haelewi iwapo mumewe anakabiliwa na shikizo la kazi za ofisi au la, kwasababu hazungumzii jambo lolote.

Hajui ni nani wa kumueleza kuhusu tatizo hili. Hivi karibuni alipatikana na maradhi ya kisukari . Madawa yanatumiwa kwa hilo. Je watu wenye kisukari wanakuwa na tabia kama hiyo kila wiki?

Kwa upande mwingine Shaijala ana dalili za anazozipata mwanamke aliyefikia umri wa kutoweza kuzaa (menopause).

Kwa ujumla, Shailaja na mume wake huwa hawafanyi tendo la ndoa hata mara moja kwa mwema.

"Sielewi iwapo ninapaswa kutuza afya yangu au kukosa bubira na kuchosha kwa mume wangu ," alisema Shailaja.

Aliwahi kusikia kuwa kipindi cha menopause hutukea kwa wanawake na wakati wanapofikia umri huu huwa na hisia zinazobadilika badilika wakati huo, lakini anasema hajawahi kusikia kwamba wanaume pia , hupitia kipindi kinachofahana na hicho.

Baada ya kushindwa kuvumilia majonzi aliyokuwa nayo, alimua kuongea na daktari ambaye alikuwa rafiki yake

Alielezea waiwasi wake kuwa anashuku huenda alikuwa na hali ya inayofahamika kama andropause na akashauriwa kupata ushauri wa daktari .

Kwa kawaida suala la kipindi cha Menopouse kinachowapata wanawake waliofikia umri wa kutoweza kujifunguliwa huzungumziwa mara nyingi. Lakini hali ya andropause inayowapata baadhi ya wanaume walio katika kipindi hicho ni nadra sana kuzungumziwa.

Lakini je wanaume pia hupitia kipindi cha hali ya kukwama kwa hedhi, menopause? Suala hili litawahi kuzungumziwa wazi kwa umma? Je kipindi hiki kinaitwaje kimatibabu ?.

Wala hata hawezi kumgusa kwa mkono Shailaja wawapo chumbani. Tatizo lilianza kuibuka katika maisha yao ya ndoa.

సంతానలేమి

Chanzo cha picha, Getty Images

Wataalamu wa tiba wanasema kuwa hatua sawa na ile anayoipitia mwanamke aliyefikia umri wa kutokuwa na uwezo wa kujifunguakwa wanaume huitwa andropause. Jarida la kitabibu linasema mara nyingi hali hii huonekana miongoni mwa wanume wenye umwi wa zaidi ya miaka 50.

Dokta Karuturi Subramaniam, daktari bingwa wa maradhi ya kisukari na homoni za mwili kutoka Rajahmundry, anasema sio sahihi hali ya andropause na ile ya menopause miongoni mwa wanawake.

"Menopause hutokea kwa wanawake wote, lakini andropause haipatikani kwa wanaume wote. Ni wachache pekee wenye hali hii ," alisema.

Alifafanua kuwa andropause huweza kusababushwa zaidi na kasoro fulani inayotokana na mtindo wa maisha, matatizo ya kiafya au hata maradhi ya kisukari na unene wa mwili wa kupindukia.

డాక్టర్ కరుటూరిసుబ్రహ్మణ్యం

Chanzo cha picha, DR KARUTURI SUBRAHMANYAM

Maelezo ya picha, Dokta Karuturi Subrahmanyam

Ni zipi dalili za andropause?

Hali ya Andropause haiwapati watu wazima wote. Andropause husababishwa na mabadiliko katika homoni za kiume ambayo hujitokeza kutokana na umri.

Nchini Uingereza jwa mfano mamlaka ya huduma za afya inasema hali ya andropause inaweza kusababishwa na uvutaji wa sigara, ukosefu wa usingizi, mlo dhaifu, kutofanya mazoezi na kukosa kujiamini .

Mambo hayo yaliungwa mkno na Dkt Karuturi Subramaniam.

Alisema dalili sawa na hizo pia zinaweza kuwapata watu wenye umri wa kati kutokana na msongo wa mawazo na wasi wasi wanaokumbana nao maishani mwao.

Homoni huchochea shauku ya kufanya tendo la ndoa miongoni mwa wanaume, mabadiliko wakati wa kipindi cha kubalehe, ukuaji wa kiakili na kimwili, kuimarika kwa mishipa, na ukuaji mwingine wa mwili.

సంతానలేమి

Chanzo cha picha, Getty Images

  • Kupungua ikwa viwango vya homoni kunaweza kuathiri ufanisi wa tendo la ndoa na kusababisha dalili zifuatazo :
  • Kuhisi kupungua kwa nguvu mwilini
  • Msongo wa mawazo,au huzuni
  • Kukosa shauku
  • Kushindwa kujiamini
  • Kushindwa kumakinika
  • Kuongezeka kwa viwango vya mafuta ya mwili
  • Kupungua kwa ugumu wa misuli
  • Kuongezeka kwa viwango vya kupumua
  • Kudhoofika kwa mifupa
  • Kupungua kwa uwezo wa ngono , na utashi
  • Kukosa usingizi
  • Kupoteza nywele za mwili
  • Kupungua kwa ukubwa wa mfuko wa mbegu za kiume
  • Kupatwa na mawimbi ya joto la mwili- Hot flashes

"Hatahivyo hali hii haimpati kila mtu mwenye umri wa zaidi ya miaka 50 . Uwezo wa viungo vya uzazi pia haupungui kabisa ," anasema dokta Karuturi Subramaniam.

Inasemekana dalili hizi mara nyingi huonekana miongoni mwa watu wenye kisukari na unene wa mwili wa kupindukia.

సంతానలేమి

Chanzo cha picha, bambam kumar jha/getty images

Kwa ujumla viwango vya homoni vinapaswa kuwa kati ya kipimo cha nanogramu gramu 250 hadi 1100 nanograms kwa desilita, kulingana na taasisi ya tiba yenye makao yake California- Faci Medical Group.

Hatahivyo kuna tofauti baina ya viwango ambavyo taasisi tofauti za tiba zinasema kuhusu kiwango chake.

సంతానలేమి

Chanzo cha picha, Getty Images

Ni ipi tiba ya hali hii ?

Wale wanaoathiriwa na dalili hizi wanasemekana kuwatemelea madaktari huku wakiwa na matatizo ya aina tofauti.

Baadhi ya wanawake wanaweza kusema tu kwamba , "Huwa hanisogelei kwa sasa ."Wakati huo ni muhimu kufahamu mzizi wa tatizo na kuutibu.

Kubaini hili, vipimo vya damu hufanywa ili kubaini viwango testosterone.

Wakati viwango vya homoni vinapoonekana kupungua, dokta Karuturi Subramaniam anasema ni muhimu kufahamu sababu ya dalili hizo bila kuamua kuwa mara moja tatizo ni andropause.

Inaweza kuponywa kwa kumpatia mgonjwa aina mbali mbali za jeli, au sindano za homoni . Hatahivyo , alionya kuwa matumizi ya sindano za homoni yanaweza kusababisha baadhi ya athari .

Mazoezi yanayofaa na mapumziko ya kutosha pia vinaweza kusaidia kutibu dalili hizi nan i vyema kuendelea kufuatilia iwapo mgonjwa ana tatizo la kisukari.

Zaidi ya hayo, tabia kama vile uvutaji wa sigara na tumbaku na unywaji wapombe pia vinapaswa kuepukwa.

Ulaji wa nyama kupita kiasi, vyakula vya sukari na vinjwaji baridi vnaweza pia kuwa hatari.

ఆకుకూరలు

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kula mboga zaidi na matunda

Kula matunda mawili makavu kama lozi, tende na korosho

Kula chakula chenye madini ya calcium, zinc, omega 3, vitamini D, ana vitamini-E.

Maziwa yenye viwango vya chini vya mafuta, mtindi, jibini, na mboga mbalimbali za kijani kibichi zinapaswa kuliwa.

Karoti, pilipili manga, nyanya, kabeji na , beetroot vinapaswa kuliwa

Ukosefu wa madini ya kutosha ya Lack zinc mwilini pia hupunguza mfumo wa kinga mwilini.

అత్యధిక పోషక విలువలు కలిగిన పదార్థాల జాబితాలో తొలిస్థానం బాదంకే దక్కింది.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Korosho ilikua miongoni mwa vyakula vyenye virutubisho vingi zaidi

Vyakula kama samaki, maini ya kuku, bata na chokoleti vinaweza kuboresha uwiano wa homoni.

Vyakula vya majini kama samaki aina ya tuna na salmon wenye kiwango kikubwa cha Omega 3 , maboga ba mbegu kama vile , flax na njugu za sabza nuts vinapendekezwa kuongezwa katika milo yetu.

Inasemekana vitamin D huwa na mchango mkubwa sana katika utengenezwaji wa homoni za testosterone zinazochochea hamu ya ngono.

Ni bora zaidi kutumia mafuta ya mizaituni

Daktari pia anasema ni vyema kula tunda katika kila mlo wa siku.

ప్రతీకాత్మక చిత్రం

Chanzo cha picha, Getty Images

Shailaja alimshawishi mume wake kumuona daktaribaada ya kuzungumza na rafiki yake wa kike. Mume wake alibadili mtindo wake wa maisha baada ya kuzungumza na daktari, alianza kufanya mazoezi .

Shailaja anasema mlo unaofaa na kubadilisha mtindo wa maisha kwa mume wake kumeonyesha mabadiliko tofauti na anasema tabia ya mume wake ya kukasirika ovyo ilipungua.

"Sasa maisha yangu ya kingono yamekuwa mazuri. Sihisi kuchoka ninapokuwa karibu na mke wangu kama siku za nyuma. Inaonekana ni kutokana na kubadilisha mtindo wa maisha."

"Movies na shikars wamerejea katika maisha yao ya awali. Tunaendelea kufuata sheria za Covid," alicheka Shailaja.