Tetesi za Soka Ulaya Jumapili 16.01.2022:Haaland, Benitez, Phillips, Rangnick, De Jong, Costa, Carlos, Lingard

m

Chanzo cha picha, Getty Images

Iliyochapishwa

Real Madrid au Barcelona watalazimika kutumia euro milioni 350 (£292m) kumsajili mshambuliaji wa Norway Erling Braut Haaland kutoka Borussia Dortmund, kiasi ambacho kinajumuisha ada ya uhamisho ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21, mshahara wa mkataba wa miaka sita na kamisheni alizolipwa baba yake na wakala Mino Raiola na baba yake.(Marca)

Everton na meneja Rafael Benitez wamekubali kuachana, huku mazungumzo yakiendelea kuhusu taarifa za kuondoka kwake. Duncan Ferguson, ambaye ni sehemu ya timu ya kocha Benitez, ameombwa kuchukua nafasi ya meneja wa muda.(90 Min)

Kiungo wa kati wa Leeds United wa Uingereza Kalvin Phillips anasakwa na Liverpool, lakini Leeds wako tayari kumwacha mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 kwenda nje ya nchi, huku Paris St-Germain, Bayern Munich na Real Madrid wakiwa miongoni mwa wawaniaji wake. (El Nacional - in Catalan)

Chelsea lazima waongeze ofa yao ya pauni milioni 33 ikiwa wanataka kumsajili Frenkie de Jong wa Barcelona. Barca wanadai euro milioni 60 (£50m) kwa kiungo huyo wa kati wa Uholanzi, 24, ambaye pia anasakwa na Bayern Munich.(El Nacional - in Catalan)

M

Mkufunzi wa muda Ralf Rangnick hajafurahishwa na kitendo cha Manchester United kusita kumuunga mkono kwenye dirisha la usajili na ana wasiwasi kuhusu ushawishi mkubwa atakaokuwa nao atakapoanza kazi yake ya ushauri kwa miaka miwili msimu wa joto.(Mirror)

Kocha wa Paris St-Germain Mauricio Pochettino amekuwa akihusishwa na kuchukua nafasi ya meneja wa Manchester United lakini, bila mazungumzo ya moja kwa moja kati ya pande hizo mbili, klabu nyingine kubwa ya Ulaya pia inavutiwa na huduma ya Muargentina huyo.(Telegraph - subscription required)

Kiungo wa kati wa Denmark Christian Eriksen, ambaye alipatwa na mshtuko wa moyo kwenye michuano ya Euro 2020 mwezi Juni, amekuwa na mbinu kutoka kwa vilabu kadhaa vya Ligi ya Premia na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 anatarajia kukamilisha kuhamia timu moja wapo mwishoni mwa juma.(Times - subscription required)

M

Mshambulizi wa Misri, Mohamed Salah anakataa kuyumbishwa na imani kwamba ana thamani ya pauni 400,000 kwa wiki kusaini mkataba mpya na Liverpool. Mkataba wa sasa wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 utakamilika msimu wa joto wa 2023.(Mirror)

Arsenal wamefanya mazungumzo yasiyo rasmi na mshambuliaji wa zamani wa Chelsea Diego Costa, 33,Anatarajia kuondoka Uhispania mwezi huu.(Goal - in Portuguese)

Newcastle United wanatarajiwa kuanza tena mazungumzo na Sevilla wiki ijayo kuhusu kumsajili beki wa kati wa Brazil Diego Carlos, 28.(90 Min)

Newcastle imekuwa na ofa ya zaidi ya euro milioni 40 (£33.4m) kumnunua beki Mfaransa mwenye umri wa miaka 20 Benoit Badiashile iliyokataliwa na Monaco.(Foot Mercato via Get French Football News)

Newcastle wanasonga mbele na majaribio ya kumsajili winga wa Napoli Robin Gosens, 27, ambaye amekuwa nje ya uwanja tangu Septemba. (Sky Sport Italia - in Italian)

M

West Ham wanakabiliwa na ushindani mkali kutoka kwa Newcastle kwa ajili ya kumnunua kiungo wa kati wa Manchester United Muingereza Jesse Lingard, ambaye mkataba wake utamalizika msimu wa joto. Lingard alicheza kwa mkopo West Ham msimu uliopita, lakini Newcastle wako tayari kulipa £3m kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 mwezi huu.(Star)

Barcelona wana nia ya kumsajili Roberto Firmino kutoka Liverpool, ambaye anataka euro milioni 20 (£16.7m) kwa mshambuliaji huyo wa Brazil mwenye umri wa miaka 30.(El Nacional - in Catalan)

Mshambulizi wa Inter Milan na Croatia Ivan Perisic, 32, anavutiwa na Chelsea, huku mkufunzi Thomas Tuchel akitaka kuongeza ulinzi katika winga wa kushoto kufuatia jeraha la mlinzi wa Uingereza Ben Chilwell, 25. (Mirror)

Atletico Madrid hawana nia ya kumuuza mshambuliaji wa Ureno Joao Felix mwenye umri wa miaka 22 mwezi Januari au msimu wa joto.(Marca)

MM

Aston Villa wanafikiria kumnunua mlinda mlango wa Coventry City Muingereza Simon Moore, 31. Meneja wa Villa Steven Gerrard anataka kuongeza ulinzi kwa mlinda mlango wa Argentina Emiliano Martinez, 29. (Football Insider)

Manchester United inamthamini mlinzi wa kati wa England Phil Jones, 29, kwa pauni milioni 15, huku Burnley na Newcastle zikiwa na nia ya kutaka kuhama.(Star)

Beki wa Uingereza Kortney Hause, 26, anatamani kujiunga tena na klabu ya utotoni ya West Ham ikiwa ataondoka Aston Villa mwezi huu.(Football Insider)

West Ham inamfuatilia mshambuliaji wa Strasbourg Mfaransa Ludovic Ajorque, 27, ambaye amefunga mabao 10 ya Ligue 1 msimu huu.(Foot Mercato - in French)

Napoli wako kwenye mazungumzo ya kumsajili beki wa kushoto wa Argentina Nicolas Tagliafico, 29, kutoka Ajax.(Sky Sport Italia - in Italian)

Wolves wanakaribia kumnasa winga wa Ureno Chiquinho mwenye umri wa miaka 21 kutoka Estoril kwa pauni milioni 3 kwa mkataba wa muda mrefu.(Athletic)