Tetesi za soka Ulaya Jumamosi 14.05.2022: Jesus, Mbappe, Griezmann, Perisic, De Jong, Bellingham

Jesus

Chanzo cha picha, Chris Brunskill/Fantasista

Iliyochapishwa

Arsenal wanajiandaa kupeleka ofa ya kati ya €50-60m to kwa ajili ya Gabriel Jesus. Manchester City inatakata kiasi hicho kwa ajili ya kumuuza Gabriel msimu huu, hata kama mkataba wake uliosalia mwaka mmoja hautaongezwa. (Fabrizio Romano)

Real Madrid are "wana jiamini kuliko wakati wowote" kwamba wanaweza kukamilisha usajili wa mshambuliaji wa Ufaransa na Paris St-Germain Kylian Mbappe, lakini nyota huyo mwenye miaka 23 hajaamua kuhusu mustakabali wake. (Fabrizio Romano)

Mbappe

Chanzo cha picha, Getty Images

Barcelona hawana mpango na Antoine Griezmann, 31, kurejea kwenye klabu hiyo kama Atletico Madrid hawataamua kubaki nae kwa mkopo mshambuliaji hiyo mfaransa. Chaguo la kwanza la Barca ni mshambuliaji wa Bayern Munich na Poland Robert Lewandowski. (Cuatro - in Spanish)

Hata hivyo, Rais wa Bayern Munich Herbert Hainer anasema Lewandowski yuko na mkataba na mabingwa hao wa Bundesliga mpaka June 2023 - na mkongwe huyo mwenye miaka 33 "atamalizia mlataba wake". (Sport Buzzer - in German)

Chelsea imefikia makubaliano ya awali ya kumsajili winga wa Croatia Ivan Perisic, 33, bure akitokea Inter Milan. (Mediaset, via Metro)

Perisic

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Perisic

Kiungo wa Barcelona na Uholanzi Frenkie de Jong, 25, anajiandaa kukataa kuhamia Manchester United, aambapo kocha wake ajaye Erik ten Hag anatarajia kutowachekea wachezaji wote wenye nia ya kuondoka Old Trafford msimu huu. (Star)

Kiungo wa England Jude Bellingham, 18, amezungumzia tetesi zinazomuhusisha kuhamia kati ya Manchester United au Liverpool kwa kuthibibitisha kwamba atasalia Borussia Dortmund msimu ujao. (Mirror)

Swansea City inakabiliana na ushindani kutoka klabu zilizopanda ligi kuu za Fulham na Bournemouth katika kumsajili kiungo wa Wales, Joe Allen, 32 kutoka Stoke City. (Wales Online)

Lukaku

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Lukaku

Mshambuliaji wa Chelsea na Ubelgiji Romelu Lukaku, 29, anasema "hataruhusu mtu kuzungumza kwa niaba yake" baada ya wakala wake Federico Pastorello kuzungumza na gazeti moja la Italia kuhusu uwezekano wa kurejea Italia. (Star)

Wakala wa mshambuliaji wa Juventus na Argentina Paulo Dybala, 28, ameelezwa yuko London kufuatilia ofa kutoka klabu za ligi kuu, ikiwemo Arsenal. (Calciomercato via Football Italia)

West Ham wako tayari kujiondoa katika mbio za kumsajili beki wa kati wa Burnley Muingereza English James Tarkowski, 29, wakitarajia mlimzi huyo kujiunga na Newcastle msimu huu. (Mirror)