Tetesi za Soka Ulaya Ijumaa 03.06.2022: Lacazette, Tielemans, Asensio, Lukaku, Lingard, Mee

Lacazette

Chanzo cha picha, Getty Images

Iliyochapishwa

Lyon wanataka kumnunua tena mshambuliaji wa Ufaransa Alexandre Lacazette, 31, kwa uhamisho huru - miaka mitano baada ya kumuuza kwenda Arsenal kwa £46.5m. (L'Equipe)

Arsenal pia wanataka kumsajili kiungo wa kati wa Ubelgiji Youri Tielemans, 25, ambaye ataondoka Leicester City msimu huu wa joto. (Fabrizio Romano, Twitter)

Manchester United watapewa fursa ya kumsajili winga wa Real Madrid Mhispania Marco Asensio, 26. (El Chiringuito - in Spanish)

Barcelona wanatarajiwa kuelekeza mawazo yao kwa mshambuliaji wa Chelsea na Ubelgiji Romelu Lukaku, 29, ikiwa hawatawea kumsajili Robert Lewandowski, mshambuliaji wa Poland mwenye umri wa miaka 33 ambaye anatazamiwa kuondoka Bayern Munich. (Mundo Deportivo)

Lukaku

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Lukaku

Mshambulizi wa Manchester City Mbrazil Gabriel Jesus, 25 na mlinzi wa Ukraine Oleksandr Zinchenko, 25, wote wanaweza kuondoka msimu huu wa joto, huku winga wa England Raheem Sterling, 27, anaweza kwenda timu nyingine ya daraja la juu. (The athletic)

Arsenal wamemfanya Jesus kuwa chaguo lao namba moja ingawa wanakabiliwa na ushindani kutoka kwa Juventus katika mbio za kumnunua mchezaji huyo wa zamani wa Palmeiras. (Mirror)

Beki wa Uholanzi Nathan Ake, 27, pia ameambiwa anaweza kuondoka Manchester City na hilo linaweza kufungua njia ya kuhamia Newcastle. (Talksports)

Beki Mholanzi Sven Botman, 22, anataka kuondoka Lille msimu huu wa joto na anasema AC Milan na Newcastle wana nia ya kumsajili. (Algemeen Dagblad, via Chronicle)

Tottenham wamepewa nafasi ya kumsajili kiungo wa kati wa West Ham kutoka Jamhuri ya Czech Tomas Soucek, huku mazungumzo kuhusu kandarasi mpya kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 yakiwa yamekwama. (Football Insider)

Roma wanamnyatia kiungo wa kati wa Uingereza Jesse Lingard, 29, mkataba wake na Manchester United utakapokamilika msimu huu, lakini West Ham na Everton miongoni mwa wanaomsarandia kiungo huyo. (Gazzetta dello Sport)

Jesse Lingard

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Jesse Lingard

Leeds United wako kwenye mazungumzo ya kumsajili beki wa kulia wa Red Bull Salzburg na Denmark Rasmus Kristensen, 24. (Sky Sports).

Burnley walioshuka daraja wanatarajia nahodha wake Ben Mee, 32, kuondoka msimu huu wa joto, na hivyo kuacha pengo kubwa katika kundi la wachezaji viongozi huku nahodha msaidizi na mlinzi mwenzake Muingereza James Tarkowski, 29, pia akitarajiwa kuondoka. (Usajili unahitajika)

Nottingham Forest iliyopanda daraja msimu huu inaweza kumnunua kiungo wa kati wa Southampton na timu ya vijana ya chini ya miaka 21 ya Jamhuri ya Ireland Will Smallbone, 22, ambaye ataruhusiwa kuondoka kwa mkopo 2022-23. (Sun)

Forest, Norwich City na Huddersfield Town wanapanga mipango ya kumsajili beki wa kushoto wa Angers raia wa Cameroon Enzo Ebosse, 23. (Football Insider)