Safari ya wahamiaji wa Uingereza kupelekwa Rwanda 'yaota mbawa', Mahakama yaingilia kati

Boeing 767

Chanzo cha picha, PA Media

Maelezo ya picha, Ndege aina ya Boeing 767 ikiwa MoD Boscombe Down, karibu na Salisbury, inadaiwa ndege hii ndiyo ilipaswa kutumika kuwasafrisha wahamiaji wa Uingereza kwenda Rwanda.
Iliyochapishwa

Safari ya kwanza ya ndege iliyopaswa kuchukua wahamiaji kutoka Uingereza hadi Rwanda ilisitishwa dakika chache kabla ya kupaa baada ya maamuzi ya kisheria jioni ya Jumanne.

Wahamiaji saba walikuwa wakitarajiwa kupelekwa katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki.

Lakini safari ya ndege hiyo ilisitishwa baada ya uingiliaji kati uliochelewa kutoka kwa Mahakama ya Ulaya ya Haki za Kibinadamu (ECHR) kusababisha changamoto mpya katika mahakama za Uingereza.

Waziri wa Mambo ya Ndani Priti Patel alisema "amesikitika" lakini akaongeza: "Maandalizi ya safari ya ndege inayofuata yanaanza sasa."

Hata hivyo, James Wilson kutoka kikundi cha kampeni cha Detention Action alisema uingiliaji kati nadra kutoka kwa ECHR "unaonyesha jinsi uwezekano wa kupelekwa wahamiaji hao Rwanda uko hatarini."

Alisema mahakama imetambua hakuna mtu anayepaswa kulazimishwa kupanda ndege hadi sera hiyo ichunguzwe kikamilifu katika kikao cha Mahakama Kuu mwezi ujao.

Kusitishwa kwa safari hiyo ndege kulifuatia siku za mabishano katika mahakama za Uingereza, na hivyo kumalizika kwa waziri wa mambo ya ndani kupata kibali cha kuanza kuwasafirisha baadhi ya watu wanaotafuta hifadhi.

Ndege aina ya Boeing 767, iliyokodishwa kwa gharama inayokadiriwa kufikia £500,000, ilitarajiwa kupaa usiku wa saa 4:30 kutoka uwanja wa ndege wa kijeshi huko Wiltshire.

Lakini hukumu kutoka kwa ECHR huko Strasbourg ya kusitisha kufukuzwa kwa mmoja wa wahamiaji hao ilitoka masaa matatu kabla ya ndege kuondoka, na kusababisha msururu wa changamoto za kisheria katika mahakama za London. Kufikia saa 4 na robo abiria wote walikuwa wameondolewa kwenye ndege, ambayo ilirudi Hispania.

Mahakama ya haki za binadamu ya Strasbourg - sehemu ya Baraza la Ulaya, ambayo bado inaihesabu Uingereza kama mwanachama, nje ya Umoja wa Ulaya - ilisema mtu mmoja raia wa Iraq anayejulikana kama KN anakabiliwa na "hatari halisi ya madhara yasiyoweza kurekebishwa" ikiwa angebaki kwenye ndege. .

Ingawa Mahakama Kuu ya London iligundua kuwa KN anaweza kurejeshwa nchini Uingereza ikiwa nia yake ya kubatilisha sera ya usafiri ya Rwanda itafaulu, ECHR ilisema hakuna utaratibu unaoweza kutekelezwa kisheria kuhakikisha kwamba anaweza kurejea baada ya kufika Afrika Mashariki.

UK

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Baadhi ya wananchi wanaopinga zoezi la kupelekwa Rwanda bila hirari kwa wahamiaji wa Uingereza

Wachambuzi wanasemaje?

Dominic Casciani, mwandishi wa masuala ya kisheria ana mtazaqmo wake kwenye sakata hili. Ilichukua zaidi ya saa moja kwa mpango mzima wa kuwasafirisha wahamiaji kupelekwa kwa hifadhi nchini Rwanda Jumanne usiku kanguka ghafla - kutokana na mfululizo wa maamuzi ya kisheria, yote yakichochewa na uamuzi mmoja kutoka Mahakama ya Ulaya ya Haki za Kibinadamu.

Abiria saba waliosalia na maagizo ya kupanda ndege ya Boeing 767 wakiota joto katika MoD Boscombe Down walionekana kama hawaji cha kufanya - lakini mahakama ya Strasbourg, ambayo ndiyo yenye uamuzi wa mwisho katika masuala ya haki za binadamu, iliamua kwamba mtu mmoja alikuwa ameibua wasiwasi wa kweli kuhusu suala hilo. Mpango huo na ukweli kwamba majaji wa Uingereza walikuwa bado hawajaangalia ipasavyo hali ya Rwanda.

Uamuzi huo, katika kesi moja tu, uliwaongoza wanaume waliobaki kukata rufaa - baadhi kwa majaji huko London. Hatimaye, maagizo yote ya kuondolewa yalitupiliwa mbali.

Hata hivyo, sera haijafa. Jambo ambalo hatujui kwa sasa ni jinsi majaji watakavyotawala watakapochunguza sera nzima ya Rwanda mwezi ujao.

Vita hivi - kati ya mawaziri, wanasheria wanaowaona kama maadui, na sasa Mahakama ya Ulaya - ndiyo kwanza inaanza.

'Maandalizi ya safari ya pili yanaanza sasa'

Mahakama ya Strasbourg pia ilisema Umoja wa Mataifa umeibua wasiwasi kwamba waomba hifadhi wa Uingereza wanaopelekwa Rwanda hawataweza kupata taratibu "za haki na zenye ufanisi" kuamua hali yao ya ukimbizi.

Na ilibainisha kuwa Mahakama Kuu ilikubali kulikuwa na masuala mazito kuhusu iwapo Rwanda ilikuwa imefanyiwa tathmini kwa usahihi kama nchi ya tatu salama.

Katibu wa Mambo ya Ndani alisema "vizuizi vinavyorudiwa vya kisheria" ni sawa na vile ambavyo serikali ilikabiliana navyo wakati wa uhamishaji mwingine, na kuongeza kuwa "wengi wa wale walioondolewa kwenye ndege hii watawekwa kwenye ndege ijayo".

Bi Patel alisema kwamba amekuwa akidumisha sera hii "isingekuwa rahisi kuwasilisha" lakini akaongeza "inashangaza sana" mahakama ya Ulaya iliingilia kati baada ya serikali kuruhusiwa kuendelea na safari za ndege na mahakama za ndani.

"Timu yetu ya wanasheria inapitia kila uamuzi uliofanywa kwenye safari hii ya ndege na maandalizi ya safari ya pili ya ndege yanaanza sasa," alisema.

Serikali ya Rwanda ilisema imesalia kujitolea katika makubaliano yake na Uingereza na "haikukatishwa tamaa" na kushindwa kwa safari ya kwanza ya ndege kuondoka.

Msemaji wake Yolande Makolo alisema: "Rwanda iko tayari kuwapokea wahamiaji hao watakapofika na kuwapa usalama na fursa katika nchi yetu."

Uingereza yenyewe inasemaje?

Boris Johnson

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Boris Johnson

Mapema siku ya Jumanne, Waziri Mkuu Boris Johnson aliliambia baraza lake la mawaziri kwamba watu wanaohujumu sera ya Rwanda "wanapendeleza kazi ya magenge ya wahalifu" na kusema serikali haitazuiliwa na sera hiyo.

Alipoulizwa na wanahabari ikiwa Uingereza itajiondoa kwenye Mkataba wa Ulaya wa Haki za Kibinadamu, ambao mahakama ya Strasbourg inauunga mkono, Bw Johnson alisema "vizuri sana inaweza kuwa muhimu" kubadili sheria.

Lakini makundi yanayounga mkono wanaotafuta hifadhi yaliitaka serikali kubadili mkondo na kutoa njia ya haki kwa watu wanaokimbia mateso kutafuta hifadhi nchini Uingereza.

Mtendaji mkuu wa Baraza la Wakimbizi Enver Solomon alisema ukweli kwamba ndege hiyo haikuweza kupaa ni "ishara ya unyama wa mpango huo" na akasema serikali inapaswa kufikiria upya mipango yake kwa kuwa na "mazungumzo ya kiutu uzima na Ufaransa" juu ya njia za kuingilia wahamiaji. .

Bwana Wilson kutoka Detention Action alisema Mahakama ya Ulaya ya Haki za Kibinadamu, iliyoanzishwa kufuatia mauaji ya Holocaust, "imefanya kile ilichoanzishwa," na kuuita "usiku wa vitabu vya historia".