Uchaguzi Kenya 2022: Kupeana mkono kulivyobadilisha matarajio ya watu wanaomuunga mkono Odinga

Bango

Chanzo cha picha, AFP

    • Author, Evelyne Musambi
    • Nafasi, BBC News, Nairobi
  • Iliyochapishwa

Wakati wa ziara ya kuzuru kitovu cha mgombea urais wa Kenya Raila Odinga, ilidhihirika wazi kuwa uamuzi wake mkubwa wa kuunda muungano na mpinzani wake mkuu, Rais anayemaliza muda wake Uhuru Kenyatta, umezaa matunda.

Barabara ya kuelekea nyumbani kwake katika mji mdogo lakini wenye shughuli nyingi wa Bondo - yapata kilomita 60 (maili 37) kutoka mji wa Kisumu kando ya ziwa - imepigwa tena lami, pamoja na barabara ya kuelekea nyumbani kwa marehemu baba yake, Mzee Jaramogi.

Makamu wa Rais wa kwanza baada ya uhuru anajulikana kwa heshima na Wakenya.

Mzee Jaramogi alihudumu katika serikali ya Jomo Kenyatta, baba yake rais wa sasa, hadi walipotofautiana, na kusababisha makamu wa rais kuwa mwanasiasa wa upinzani na kufungwa mwaka 1969 kwa miezi 18.

Kilianza kipindi kirefu cha uadui kati ya familia hizo mbili, ambao ulikamilika mwaka 2018 kwa kupeana mkono kati ya Bw Odinga na Bw Kenyatta.

"Barabara hizo mbili zilitengenezwa baada ya kupeana mkono. Tuna matumaini kwamba lami itapanuliwa hadi katika vijiji vingine ikiwa [Bw Odinga] atakuwa rais," mmiliki wa karakana Isaac Omondi alisema, akionesha kwamba Bondo tayari imepata "kuinua uso" mashimo yaliyowekwa na mfumo wa mifereji ya maji kuboreshwa.

Nyumba ya Bw Odinga mwenye umri wa miaka 77 inalindwa vikali na maafisa waliojihami, kama ilivyo kawaida kwa kila mgombea wa kiti cha urais wakati wa maandalizi ya uchaguzi.

Kuchungulia ndani kunaonesha jumba kubwa lililo na ukumbi uliopanuliwa kamili na nguzo kubwa.

Katika kona ya mbali ya ardhi yake kuna Kanisa la Lego Maria, chipukizi lililoanzishwa na Waafrika wa Kanisa Katoliki la Roma.

Nani yuko kwenye kinyang'anyiro cha kuiongoza Kenya ?

Fahamu zaidi kuwahusu wagombea urais wa Kenya

Chagua mgombea ili kutazama wasifu wake

Raila Amollo Odinga

Muungano wa Azimio la Umoja

  • Mgombea huyo mwenye umri wa miaka 77 ni mhandisi aliyesomea Chuo Kikuu cha Ufundi cha Magdeburg (sasa kinajulikana kama Chuo Kikuu cha Otto-von-Guericke Magdeburg) nchini Ujerumani.
  • Anawania kiti cha urais kwa tikiti ya Azimio la Umoja One Kenya Coalition Party.
  • Hili litakuwa jaribio lake la tano baada ya kugombea katika: 1997, 2007, 2013 na 2017.
  • Bw Odinga alikuwa mmoja wa wapiganiaji wa demokrasia ya vyama vingi nchini Kenya. Alikamatwa, akafungwa na wakati fulani akaenda uhamishoni kwa sababu ya kupigania haki hiyo
  • Aliwahi kuwa Waziri Mkuu, kuanzia 2008-2013.
  • Odinga alihusika kufanikisha miradi mikubwa iliyotekelezwa na serikali ya Kibaki, kama vile miradi ya umeme vijijini na barabara.
  • Kuafikia ukuaji wa uchumi wa tarakimu mbili kupitia uwekezaji katika biashara ndogo ndogo na sekta ya viwanda.
  • Utoaji wa huduma bora za afya kwa wote.
  • Utoaji wa vifaa vya michezo na burudani kwa ukuaji wa kimwili, kiakili, kijamii, kimaadili na maendeleo ya watu.
  • Kufuatia jaribio la mapinduzi ya Agosti 1, 1982, Raila Odinga alikamatwa na kukabiliwa na mashtaka kadhaa, yakiwemo ya uhaini ambayo alizuiliwa bila kufunguliwa mashtaka. Tume ya Ukweli ya Haki na Maridhiano iliambiwa mwaka 2011 kwamba Odinga alikuwa na mawasiliano na mpangaji mkuu wa mapinduzi hayo. Odinga amekana kuhusika kila mara. - Makavazi ya Kitaifa ya Kenya.

William Samoei Ruto

Muungano wa Kenya Kwanza

  • Mgombea huyu mwenye umri wa miaka 55 ana Shahada ya Uzamifu/PhD katika Ikolojia ya Mimea na BSc katika Botany na Zoology kutoka Chuo Kikuu cha Nairobi.
  • Anawania kiti cha urais kwa tikiti ya chama cha United Democratic Alliance ( chenye mafungamano na Kenya Kwanza).
  • Aliongoza Vuguvugu la vijana la Youth for Kanu '92 (YK'(92).
  • Wizara yake iliorodheshwa kama inayofanya bora zaidi serikalini alipokuwa Waziri wa Kilimo.
  • Alihudumu kama Naibu Rais wa kwanza wa Kenya chini ya katiba mpya ya 2010.
  • Alihudumu kama mbunge wa eneo bunge la Eldoret Kaskazini kuanzia 1997-2007.
  • Kutenga $424 milioni kila mwaka kwa biashara ndogo ndogo za kati.
  • Kuanzisha mfuko wa elimu wa kitaifa ili kukidhi gharama zisizo za masomo.
  • Tekeleza kikamilifu sheria ya usawa wa kijinsia ya thuluthi mbili katika uteuzi wa kisiasa na kutenga nusu ya baraza lake la mawaziri kwa wanawake.
  • Mnamo 2008, Mahakama Kuu ya Kenya iliamuru Naibu Rais William Ruto kusalimisha shamba la ekari 100 na kulipa $ 62,500 kwa Adrian Muteshi, mkulima ambaye alimshtaki kwa kuchukua mali hiyo baada ya uchaguzi wa 2007. - Kenya Law
  • Mnamo 2011, Bw Ruto alikabiliwa na kesi kwa makosa matatu dhidi ya binadamu: Mauaji, uhamisho wa watu kwa lazima na mateso ya watu katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu. Miaka mitano baadaye mahakama ilisitisha kesi hiyo kwa msingi kwamba - ushahidi wa upande wa mashtaka ulikuwa dhaifu. -ICC

George Wajackoyah

Chama cha Roots

  • Profesa huyo mwenye umri wa miaka 61 ana shahada ya uzamili katika sheria kuhusu maendeleo kutoka Chuo Kikuu cha Warwick na shahada ya uzamili , sheria (sheria za Marekani kutoka Chuo Kikuu cha Baltimore.
  • Bw Wajackoyah anawania kiti cha urais kwa tiketi ya Chama cha Roots Party.
  • Alihudumu kama Inspekta katika idara ya usalama ya Special branch wakati wa utawala wa marehemu Rais Daniel Moi kabla ya kulazimika kutorokea ng'ambo ili kuepuka kufunguliwa mashtaka na mamlaka.
  • Yeye ni mshirika katika kampuni ya mawakili aliyoianzisha mwaka wa 2018.
  • Alifunnza somo la sheria na uchumi katika vyuo vikuu vya Marekani, Uingereza na Kenya.
  • Kuhalalisha matumizi ya kiviwanda ya bangi
  • Badilisha siku za kazi hadi Jumatatu hadi Alhamisi.
  • Huduma ya afya ya bure na msaada kwa wazee, walio hatarini na wajawazito

David Mwaure Waihiga

Chama cha Agano

  • David Mwaure anawania kiti cha urais kwa tiketi ya Chama cha Agano.
  • Ni kiongozi wa Chama cha Agano.
  • Alihitimu na shahada ya sheria kutoka Chuo Kikuu cha Nairobi na ana Shahada ya Uzamili katika masomo ya uongozi.
  • Yeye ni wakili mkuu na amehudumu kama mwanasheria kwa zaidi ya miongo mitatu.
  • Ana kampuni ya uwakili na amewania viti mbalimbali vya kisiasa.
  • Ilianzishwa chama cha Agano mwaka 2006.
  • Kupambana na ufisadi uliokithiri.
  • kuunda nafasi za ajira.
  • Kurejesha mali ya Kenya iliyofichwa nje ya nchi.

Pata maelezo zaidi kuhusu sera za wagombea urais hapa

Wenyeji walisema Mzee Jaramogi ni mali yake na mwanawe alitoa shamba hilo kwa ajili ya kanisa ambalo majirani hufika kuabudu.

Nyumba ya baba yake iko wazi kwa umma na imegeuzwa kuwa jumba la makumbusho linalohifadhi historia ya akina Odinga, jamii yao ya Waluo, na Kenya kwa ujumla.

Familia ya Odinga imejihusisha na siasa tangu vita dhidi ya ukoloni

Chanzo cha picha, VIOLA KOSOME

Inajumuisha vitu vya binafsi vya Mzee Jaramogi, kama vile kofia zake za kitambo, fimbo, chupa tupu ya mvinyo anayoipenda Waziri Mkuu, sare zake za gereza kabla ya uhuru na gramafoni mbili.

Upande wa kulia kabisa karibu na lango kuu la jumba la makumbusho, kuna nyumba ya kwanza ambayo Bw Odinga alijenga kwa mbao.

"Bw Odinga aliijenga kwa haraka kabla ya kurejea Ujerumani [mwisho wa miaka ya 1960] kwa masomo yake.

Baba yake aliweka sharti kwamba alihitaji kujenga nyumba na kuoa kabla ya kurejea Ujerumani," anayetunza jumba la makumbusho Mercellus Otieno alisema.

Katika jumba la makumbusho kumetundikwa picha za marais wanne wa Kenya.

Uchaguzi wa Kenya 2022: Vyama vinakuahidi nini?

Chagua suala ambalo linakuvutia

Sera za kila chama

  • Azimio La Umoja One Kenya Coalition

  • Roots Party of Kenya

  • Chama cha Agano

  • Kenya Kwanza Alliance

Mwongozo huu ni muhtasari wa sera kuu zinazotolewa na kila chama.

Pata maelezo zaidi kuhusu wagombea urais wa Kenya hapa

End of Uchaguzi wa Kenya 2022: Vyama vinakuahidi nini?

Nafasi imeachwa kwa ya tano. Wengi wa Bondo wanatumai kuwa baada ya uchaguzi wa Agosti 9, kutajazwa na picha ya Bw Odinga - sio ya mpinzani wake mkuu, Naibu Rais William Ruto.

Haya pia ndiyo matumaini ya Bw Kenyatta, ambaye - baada ya kumshinda Bw Odinga katika chaguzi mbili zilizozozaniwa vikali - anamuunga mkono kama mrithi wake.

Rais Uhuru Kenyatta anamfanyia kampeni aliyekuwa hasimu wake Raila Odinga (kulia)

Chanzo cha picha, Getty Images

Wakosoaji wa Bw Odinga wanasema amekuwa mlaini katika ukosoaji wake wa ufisadi serikalini tangu kupeana mkono, huku Bw Ruto akitoa mapatano yao kama jaribio la "nasaba" mbili za kuunganisha mamlaka.

Lakini kuhusu wafuasi wa "Baba" - au Baba, kama Bw Odinga anavyorejelewa kwa upendo - wanahusika, anastahili kuongoza Kenya kwani amekuwa na jukumu kubwa katika kampeni ya kukomesha utawala wa chama kimoja, na kuibiwa- kwa maoni yao - katika chaguzi nne za vyama vingi tangu wakati huo.

"Baba amepigania demokrasia humu nchini. Kwa sababu yake tumeona serikali zikidhibitiwa.

Ninajivunia sana na nina matumaini kuwa atakuwa rais ajaye," Bw Omondi alisema.

Huku hali mbaya ya uchumi na ukosefu wa ajira zikiwa suala kubwa kwa Wakenya, manifesto ya Bw Odinga imejikita zaidi katika utengenezaji na uanzishaji wa viwanda ili kubuni nafasi za kazi.

Pia ameahidi kaya milioni mbili zenye uhitaji posho ya kila mwezi ya shilingi 6,000 za Kenya ($50; £40) kutoka kwa hazina mpya ya hifadhi ya jamii iwapo atachaguliwa kuwa rais.

Lakini Bw Omondi, alipokuwa akirekebisha injini ya gari bovu katika karakana yake, alisema kuwa wakazi wengi wa Bondo hawataki zawadi.

Uchaguzi Kenya 2022:Unaweza pia kusoma

"Hatutaki pesa za bure. Tunataka kufanya kazi kwa bidii kwa pesa zetu. Tunachohitaji afanye ni kuhakikisha sekta isiyo rasmi inasaidiwa kwa sababu inaajiri watu wengi," aliongeza kijana huyo mwenye umri wa miaka 46.

Sekta ya uvuvi ni biashara kubwa mjini Kisumu

Chanzo cha picha, VIOLA KOSOME

Mwaka jana bandari na reli katika kaunti ya Kisumu zilifufuliwa pamoja na mtandao mpya wa barabara magharibi mwa Kenya - maendeleo yaliyokaribishwa na dereva wa lori John Atwoto.

"Bandari imeongeza mahitaji ya malori hapa. Kufikia [miji ya] Kakamega na Kitale ni rahisi sasa na hii imetuokoa muda mwingi barabarani," alisema.

Kupeana mkono pia kumepunguza uhasama kati ya Waluo na Wakikuyu, kabila ambalo Bw Kenyatta anatoka.

Mmiliki wa mgahawa wa Kikuyu, Benjamin Mwangi, alisema kuwa tofauti na chaguzi mbili zilizopita, ambapo alihofia ghasia, hataondoka Kisumu wakati huu.

Bw Odinga ameongeza hisia zake za usalama kwa kumchagua Mkikuyu - Martha Karua, ambaye aliwahi kuhudumu katika serikali ya marehemu Mwai Kibaki kama waziri wa sheria - kama mgombea mwenza wake.

"Sioni mapema vurugu. Sisi Wakikuyu tuna Martha Karua kama naibu wa Odinga kwa hivyo tuko katika serikali yake [ikiwa atashinda]," Bw Mwangi alisema.

Tofauti na baadhi ya Wakalenjin - kabila ambalo Bw Ruto anatoka - wanaondoka Kisumu.

Silas Lelei, 25, anayefanya kazi za machinjio alisema mkewe na mtoto tayari walikuwa wamesafiri hadi nyumbani kwao katika eneo la asili la Bw Ruto huko Eldoret.

Anapanga kufunga biashara yake na kujiunga nao muda mfupi kabla ya uchaguzi, na atarejea tu baada ya matokeo kutangazwa na mizozo yoyote kutatuliwa. "Siwezi kukaa hapa.

Sijisikii salama. Nitafunga tarehe 1 Agosti hadi baada ya uchaguzi," alisema huku akikata kipande cha nyama kwa mteja.

Iwapo Bw Odinga atashinda, itakuwa ni wakati wa fahari kubwa kwa jamii yake kwani atakuwa Mjaluo wa kwanza kuwa rais.

Kwa Lucas Obwar, mtengeneza matairi katika jiji la Kisumu, ushindi huo utarahisisha Wajaluo kupata kazi katika sekta ya umma.

Lucas Obwar anaamini kuwa jamii ya Wajaluo inakabiliwa na ubaguzi wa kikabila

Chanzo cha picha, VIOLA KOSOME

"Tunapotuma maombi ya kazi katika mashirika ya kitaifa, hatupati kwa sababu hatujawahi kuwa na rais wa kuweka jamii yetu juu," Bw Obwar alisema.

Uvuvi ni shughuli kuu ya kiuchumi katika kaunti ya Kisumu na wakazi wanatumai kuwa urais wa Odinga hatimaye utafanya kiwanda cha kusindika samaki kuwa kweli.

"Sekta ya usindikaji itaunda nafasi za kazi na kuongeza mapato," mkazi Nelson Adul alisema.

Kuna mzaha nchini Kenya kwamba samaki hugharimu zaidi mjini Kisumu kuliko kwingineko - na sahani ya samaki wa kukaanga kutoka kwa wanawake wanaouza kando ya ziwa ilikuwa mara nne ya inavyotarajiwa.

Wavuvi katika ufuo wa Dunga, kama Denis Morio, waliwalaumu wafanyabiashara wa kati kwa hili na "kupunguza mapato yetu".

Alisema vifaa katika kiwanda cha usindikaji vitarahisisha kufungia samaki wao ili wapate muda zaidi wa kujadili bei nzuri, na chaguzi za kujaza samaki nje ya nchi.

Jiji la Kisumu pia lilikuwa nyumbani kwa kiwanda cha kusaga pamba, Kicomi, na kiwanda cha sukari, Miwani.

Kampuni zote mbili ziliharibiwa na usimamizi mbaya. Maelfu ya watu wakawa hawana kazi.

Kitongoji duni cha Obunga karibu na kiwanda chakavu cha Kicomi kina nyumba zilizojengwa kwa mabati na nyingine zimeezekwa kwa matope.

Hapa ndipo wanaishi wafanyakazi wa zamani wa kiwanda waliogeuka kuwa wachuuzi.

Isaiah Onyango, 58, anakumbuka nyakati ambapo kiwanda cha pamba kilikuwa na zamu tatu za kazi.

"Nyumba za kupangisha zilikuwa biashara iliyositawi. Vijana walikuwa wakipata kazi mara tu baada ya shule," alisema, huku akielezea matumaini kwamba Bw Odinga angenyakua urais - na kwamba Kisumu pia ingeibuka baada ya kile anachoamini kuwa miongo kadhaa kupuuza mpaka 'handshake' 'maarufu.

Election branding