Tetesi tano kubwa jioni hii

th

Chanzo cha picha, Getty Images

Iliyochapishwa

Je, tunajua nini hadi sasa kuhusu habari kubwa ya leo kuhusu Manchester City?

Ligi ya Premia imeishtaki Manchester City kwa ukiukaji zaidi ya mara 100 wa sheria zake za kifedha kufuatia uchunguzi wa miaka minne.

Imeipeleka klabu hiyo kwa tume huru kwa madai ya kukiuka kanuni kati ya 2009 na 2018.

City pia inashutumiwa kwa kutotoa ushirikiano tangu uchunguzi huo uanze Desemba 2018.

Klabu hiyo inasema inashangazwa na mashtaka hayo, ina "ushahidi usiopingika" unaounga mkono kesi yake na "inatarajia suala hili kusitishwa mara moja na kwa wote."

Iwapo klabu itapatikana na hatia ya makosa hayo, tume inaweza kutoa adhabu ikiwamo faini, kukatwa pointi na hata kuifukuza klabu kwenye Ligi Kuu.

th

Chanzo cha picha, Getty Images

Leeds United imethibitisha kuwa kocha mkuu Jesse Marsch amevuliwa majukumu yake.

Jesse alijiunga na klabu hiyo Februari 2022 na alisaidia sana kuiweka klabu hiyo kwenye Ligi ya Premia siku ya mwisho ya msimu uliopita.

Rene Maric, Cameron Toshack na Pierre Barrieu pia wataondoka katika klabu hiyo.

'Tungependa kumshukuru Jesse na wafanyikazi wake wa chumba cha nyuma kwa juhudi zao na tunawatakia heri kwa siku zijazo.

Mchakato wa kuteua kocha mkuu mpya unaendelea na tutaendelea kuwasasisha wafuasi katika siku zote zijazo.'

th

Chanzo cha picha, Getty Images

Meneja wa Arsenal Mikel Arteta anasema jibu lake kwa The Gunners kushindwa 1-0 na Everton ni kuwaambia wachezaji wake "anawapenda zaidi" kuliko alivyokuwa kabla ya mchezo.

th

Chanzo cha picha, Getty Images

Jonny Williams anasema Wales inaweza kufanya kitu maalum tena katika kufuzu kwa Ubingwa wa Ulaya licha ya kustaafu kwa Gareth Bale.

Kiungo mshambuliaji wa Swindon Town Williams, 29, ana hakika kwamba timu ya Rob Page inaweza kuimarika wakati mechi za kufuzu kwa Euro 2024 zitakapoanza Machi.

"Nadhani itabidi tusubiri kwa muda mrefu kuona Gareth Bale mwingine," alisema. "Kujaribu kuchukua nafasi yake, kwa kile alichofanya kwa Wales, ni vigumu sana kwangu.

TH

Chanzo cha picha, Getty Images

Meneja wa Manchester United hamesifu ari ya timu yake huku wakishikilia na kuwalaza Crystal Palace 2-1 kwenye uwanja wa Old Trafford licha ya kadi nyekundu ya Casemiro kipindi cha pili.